Mambo Helsinki?

Hamna mkazi wa jiji atakaeachwa nyuma!

Kuelekea usawa kati ya wakazi wa Helsinki na kati ya vitongoji vyake.

Hivi umewahi kujiuliza kama maisha yako hapa Helsinki yanaweza kuwa bora kuliko yalivyo sasa? Upatikanaji bora wa mandhari za asili, nyumba za bei nafuu zaidi, huduma za karibu za mitaa, aina mbalimbali za michezo na shughuli ambazo watoto wako wanapenda kufanya?

Au umeridhika na jinsi mfumo wa usafiri wa umma unavyofanya kazi vizuri, uzuri na ubora wa shule, urahisi wa kupata huduma bora za afya ya umma, na jinsi mashine ya kuondoa theluji zinavyofanya kazi usiku kucha ili kuhakikisha uraisi wa maisha kwako na wapendwa wako?

Ikiwa huwezi kusubiri mpaka mawazo yako ya namna ya kuboresha jiji kutekelezwa, au unataka kuhakikisha huduma za sasa zinaendelea katika siku zijazo, jiunge nasi tunapojaribu kufanya hii nyumba yetu ya pamoja, Helsinki yetu, iwe yenye urafiki zaidi, yenye kufurahisha na usawa zaidi. Kwa kila mtu.

Jina langu ni Arvind Ramachandran. Mimi ni mhamiaji kutoka India na nimeishi Helsinki kwa miaka 6 sasa. Mimi kielimu ni Msanifu Majengo (Architect) na Mtaalam wa Mipango Miji (Urban Planner), mimi pia ni a mwakilishi wa wafanyakazi katika sehemu yangu ya sasa ya kazi. Nje ya kazi, huwa ninafanya kazi za harakati kwenye masuala ya usawa na haki za binadamu, kuandaa matukio yanayojenga jamii, na kidogo kidogo katika burudani ya ucheshkeshaji (stand-up comedy).

Ninagombea uwakilishi/udiwani katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2021 kupitia Chama cha The Left Alliance katika jimbo la uchaguzi la Helsinki. Miji ni shauku yangu, na ninatarajia kushirikiana na kundi tofauti na lililohamasishwa la wakazi wa Helsinki ili kuleta mabadiliko katika namna ambavyo jiji letu linabuniwa, linajengwa na linavyoendeshwa.

Lengo kuu la kampeni hiyo ni kupunguza tofauti katika usawa wa kijamii jijini, kati ya wakazi wake na kati ya vitongoji vyake. Tunalenga katika upatikanaji wa jiji ambalo ni kwa ajili ya wakazi wote, hasa wale ambao mara nyingi hupuuzwa, kama vile watoto, vijana, wazazi wasio na mwenza (single parents), wasio na ajira, wazee, wale wenye asili tofauti, walio wachache kijinsia (gender and sexual minorities), watu wenye ulemavu, wale wenye asili ya mataifa ya nje na wasio na makazi.

Tutafanikisha hili kwa:

Kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi jijini kote, kwa kuzingatia maeneo yaliyohifadhiwa

Kupunguza athari za kimazingira za muda mfupi na mrefu katika maendeleo ya jiji

Kukuza hisia za kuwa sehemu ya jiji miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu wanaoishi jijini

Kusaidia wale wanaonyanyapaliwa na jamii kwa sababu ya hali ya mtu binafsi au changamoto za kimuktadha

Katika kurasa hizi zimewasilishwa maono ya jiji litakalo fanya kazi kwa wengi, na sio wachache tu. Pia utapata taarifa za jumla kuhusu uchaguzi ujao wa manispaa nchini Ufini.

Unakaribishwa sana kujiunga nasi katika safari hii ya pamoja kuelekea mji wa Helsinki ulio rafiki, wenye kuburutisha wote na wenye usawa kwa wote!

 

Fuatilia, saidia na shiriki katika kampeni kupitia kurasa hizi hapa chini:

https://www.arvindramachandran.com
https://www.facebook.com/arvindsome
https://www.instagram.com/arvindrchn

Changia kampeni kupitia:

https://www.arvindramachandran.com/donate

Natanguliza shukrani zangu za awali na natazamia kwa hamu kufanya kazi na wewe!